7 Mei 2025 - 21:46
Source: Parstoday
Kansela mpya wa Ujerumani aionya Marekani iache kuingilia siasa za ndani

Kansela mpya wa Ujerumani, Friedrich Merz, leo Jumatano ameionya Marekani dhidi ya kuingilia siasa za ndani za nchi yake.

Katika mahojiano na televisheni ya ZDF, Merz amesema: "Ningependa kuhimiza na kuishauri serikali ya Marekani iache siasa za ndani za Ujerumani ziwe suala la ndani ya Ujerumani na kimsingi ikae mbali na masuala haya ya kisiasa."

Merz amesema serikali ya Marekani lazima "ijiepushe" na siasa za ndani za Ujerumani, na kuongeza kuwa anatarajia kufanya mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani, Donald Trump Alhamisi.

Ameongeza kuwa bado hajamfahamu Trump binafsi, lakini atazungumza naye "kwa uwazi."
Merz amesisitiza kwamba yeye mwenyewe hakuwahi "kuingilia kampeni za uchaguzi za Marekani na kuchukua upande mmoja."
Kansela Merz ameikosoa serikali ya Marekani kwa kueneza "maoni ya kipumbavu kuhusu Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani."

Alipoulizwa kuhusu msaada wa Marekani kwa chama cha siasa kali cha Alternative for Germany (AfD), amesema: "Nimekuwa na hisia kuwa

Marekani ina uwezo wa kutofautisha kati ya vyama vya misimamo mikali na vyama vya kisiasa vya msimamo wa kati."

Wawakilishi wa serikali ya Marekani mara kwa mara walikisaidia chama cha AfD wakati wa kampeni za uchaguzi, na mshirika wa Trump, Elon Musk, alifanya mahojiano na kiongozi wa AfD, Alice Weidel.
Karibuni, Ikulu ya Marekani ilikosoa vikali serikali ya Ujerumani kwa kuorodhesha AfD kama chama cha siasa kali za mrengo wa kulia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha